Project hii imependeza sana kutokana na mwonekano wa picha ulikuwa ni mzuri,
Moja ya jambo linalofanya picha yoyote ile ipendeze (ya kuchorwa) ni mwonekano mzuri wa ile picha ambayo unahitaji ichorwe! Nikiwa na maana ile ambayo umejipiga/umepigwa nayo picha
Kwa ushauri tu; kama unataka picha yako ichorwe na itoke (mchoro) katika mwonekano mzuri basi hakikisha unapiga picha yenye ukubwa wa kuanzia MegaBites (MB) 3-15 !
hii inasaidia sana kuweza kuona vitu vingi wakati nikifanya kazi ya kuchora!
Karibuni sana wadau!
Juu, picha ikiwa tayari katika frame yake na chini hapa..ni picha ikiwa imekamilika na ikiwa inawekewa cover (matt) kwaajili ya kuzuia isisuguane na kioo wakati wa kufunga/matumizi
yeah...inapendeza sana ikiwa katika mazingira ya nyumbani ama ofisini!
picha hapa chini; ikinionyesha nimeshika picha husika baada ya kukamilika na kabla sijaituma kwa mhusika na mpendwa wangu kutoka instagram aliyevutiwa na shughuli zangu
tembelea ukurasa wangu wa instagram uone baada ya kuupokea alivyoiweka picha yake sehem nzuri na kunitumia video yake!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni