Jumatano, 14 Machi 2018

Project 3

Karibu tena mdau na kama ni mgeni katika blog hii unakaribishwa kwa mikono yote miwili! 
Kwa Mara nyingine tena nimepata kazi kutoka kwa wakili jebra /advocate_jebra kama anavyotumia jina hili katika mtandao wa Instagram.
Ni mwanaharakati na mwanasheria,

Kwa Mara ya kwanza nimeanza kazi hii kwa kutumia rangi na kwa mtazamo tu naona inapendeza sana na kazi hii imepokelewa vyema sana na nyinyi wadau na wapenzi wa kazi hizi za kisanaa,  ni heshima sana kwangu na kwenu pia kwa ushauri wenu na nategemea mawazo yenu katika uboreshaji wa kazi hii

Hii ni hatua ya pili ambapo hatua ya kwanza ilikuwa ni kuchora frame ya picha na kwa bahati mbaya sijafanikiwa kuipata ile picha ya mwanzo

Jumanne, 6 Machi 2018

Uchoraji project 2

Project hii imependeza sana kutokana na mwonekano wa picha ulikuwa ni mzuri,
Moja ya jambo linalofanya picha yoyote ile ipendeze (ya kuchorwa) ni mwonekano mzuri wa ile picha ambayo unahitaji ichorwe! Nikiwa na maana ile ambayo umejipiga/umepigwa nayo picha
Kwa ushauri tu; kama unataka picha yako ichorwe na itoke (mchoro) katika mwonekano mzuri basi hakikisha unapiga picha yenye ukubwa wa kuanzia MegaBites (MB) 3-15 !
hii inasaidia sana kuweza kuona vitu vingi wakati nikifanya kazi ya kuchora!
Karibuni sana wadau!

Juu, picha ikiwa tayari katika frame yake na chini hapa..ni picha ikiwa imekamilika na ikiwa inawekewa cover (matt) kwaajili ya kuzuia isisuguane na kioo wakati wa kufunga/matumizi
yeah...inapendeza sana ikiwa katika mazingira ya nyumbani ama ofisini!
picha hapa chini; ikinionyesha nimeshika picha husika baada ya kukamilika na kabla sijaituma kwa mhusika na mpendwa wangu kutoka instagram aliyevutiwa na shughuli zangu
tembelea ukurasa wangu wa instagram uone baada ya kuupokea alivyoiweka picha yake sehem nzuri na kunitumia video yake! 

Jumatatu, 5 Machi 2018

Uchoraji

Karibu sana rafiki zangu katika kazi za uchoraji kwenye ukurasa wangu na waweza toa maoni yako na hata kunitafuta kwaajili ya kufanya kazi mbalimbali popote utakapohitaji

pia waweza nitafuta kwa njia ya #watsapp ama kunipigia simu 0692107120